Barcelona Yaizalilisha Madrid, Yaitandika Mabao 3-0

KLABU ya Barcelona imeipa kichapo cha bao 3-0 mahasimu wao Real Madrid katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka nchini Hispania, maarufu kama LaLiga Santada.

Katika mchezo huo wa kusisimua na ulioshuhudiwa na mamilioni ya watu duniani kote, hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika timu zote zilikuwa hazijafungana kwani kila timu ilikuwa inafanya mashambulizi na ku-defence.

Mambo yalibadilika kunako kipindi cha pili ambapo dakika ya 54 Louis Suarez aliiandikia Barcelona bao la kwanza baada ya kumalizia krosi ya Rakitic na kuwaacha Madrid wakiduwaa.

Dakika 9 baadaye ikatokea piga nikupige kunako lango la Madri ambapo ilipelekea Dani Carvalhal kuushika mpira uliokuwa ukizama golini kwao hivyo akatwangwa kadi nyekundu kisha refa akaamua upigwe mkwaju wa penati. Messi kama kawaida yake aliachia mkwavu mkali uliomshinda Navas na kuzama langoni hivyo kuiandikia Barca bao la 2 dakika ya 64.

Katika dakika za nyongeza, Barcelona wakapachika tena bao la 3 kupitia kwa Vidal aliyeachia mkwaju mkali hivyo kufanya mchezo umalizike kwa matokeo ya 3-0.

 

  • Real Madrid team: Keylor Navas; Carvajal, Varane, Sergio Ramos, Marcelo; Casemiro (Asensio), Modric, Kroos, Kovacic (Bale); Cristiano Ronaldo, Benzema (Nacho)
  • Substitutes: K Casilla,  Theo, Lucas, Isco

  • Barcelona team: Ter Stegen; Sergi Roberto, Pique, Vermaelen, Alba; Busquets, Rakitic, Iniesta (Semedo); Paulinho, Messi, Suarez
  • Substitutes: Cillessen, Denis Suarez, Mascherano, Digne, Andre Gomes, Vidal.

MSIMAMO WA LALIGA

Team P GD Pts
1 Barcelona 17 38 45
2 Atlético de Madrid 17 17 36
3 Valencia CF 16 20 34
4 Real Madrid 16 16 31
5 Sevilla 17 -2 29
6 Villarreal 16 3 24
7 Eibar 17 -7 24
8 Getafe 17 6 23
9 Real Sociedad 17 2 23
10 Girona 17 -5 23
11 Athletic Club 17 -1 21
12 Leganés 16 -2 21
13 Real Betis 17 -6 21
14 Espanyol 17 -7 20
15 Celta de Vigo 16 3 18
16 Levante 17 -7 18
17 Alavés 17 -12 15
18 Deportivo de La Coruña 16 -13 15
19 Málaga 17 -18 11
20 Las Palmas 17 -25 11