Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete amesema kwa sasa Africa inatakiwa kujiuliza kama miundo mbinu inayojengwa Leo inaendana na mahitaji ya uchumi wa siku zijazo kwasababu ifikapo mwaka 2030 kutakuwa na zaidi ya vijana milioni 12 wataingia katika soko la ajira
Amesema ongezeko hilo linaweza kuongeza changamoto za ukosefu wa ajira ,umasikinizkukatatamaa kwa vijana kunahatarisha utulivu wa kijamii
Dk Kikwete amesema ifikapo mwaka 2050 Bara la Afrika linatarajiwa kuwa na zaidi ya robo ya watu wote duniani hivyo kunahitajika kuwepo kwamiundo mbinu yenye maandalizi ya kutosha
Amesema kwa sasa uwekezzaji katika elimu unapaswa kwenda sambamba na uwekezzaji katika miundo mbinu ili kuzalisha nguvu kazi yenye maalifa ,ubunifu na uwezo.

Amesema mafanikio ya miradi hayapaswi kupimwa kwa ukubwa au idadi ya miundo mbinu inayojengwa pekee bali kwa kiwango ambacho kitachangia kuboresha maisha ya Wananchi kupitia ajira,kuvutia wawekezaji,kuinua ustawi wa jamii na kuchochea biashara
Waziri wa Fedha wa Fedha Khamisi Musa Omari amesema mkutano wa Africa50 ulikuwa na faida kubwa kwaTanzania kwasababu tumeweza kusaini mikataba mitatu yenye manufaa kwetu
Amesema pamoja na mambo mengi ya yaliyo jadiliwa na kisainiwa kwa mikataba mbalimbali ,Pia umeleta pamoja pamoja wafadhili wa miundo mbinu na Taasisi za kifeha za kimataifa kama DFI na watu wa sekta binafsi ambao wapo tayari kuwekeza kwenye miundo mbinu.


