Shirikisho la Soka duninai (FIFA) limethibitisha kuwa zaidi ya tiketi milioni moja za Kombe la Dunia zimeombwa na mashabiki kupitia mtandao wake katika kipindi cha saa saba pekee tangu zianze kuuzwa.

Taarifa zinasema kuwa mashabiki wengi waliojitokeza kununua tiketi hizo kupitia mtandao huo ni kutoka katika nchi za Brazil, Argentina, Marekani na Uingereza.

Taarifa zaidi zilisema kuwa mashabiki wa soka wanaohitaji kununua tiketi hizo wanaweza kuendelea kuomba tiketi hizo kupitia mtandao wa FIFA hadi Oktoba 10, mwaka huu.

Halmashauri ya Utalii Brazil imetoa wito kwa FIFA na wamiliki wa hoteli nchini humo kupunguza gharama za huduma na bidhaa zao kwa wateja kuepusha kuchafua jina la nchi hiyo.

Gharama hizo zimepanda maradufu tangu matayarisho ya Kombe la Dunia yashike kasi.

Taarifa zaidi zilisema kuwa mashabiki wa soka wanaohitaji kununua tiketi hizo wanaweza kuendelea kuomba tiketi hizo kupitia mtandao wa FIFA hadi Oktoba 10, mwaka huu.

954 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!