Hatimaye Klabu ya Soka ya Chelsea ya Uingereza  imekubali kulipa kiasi cha pauni millioni 30 sawa na bilioni 75 za kitanzania, kumsajiliwa kiungo mchezaji Willian Borges da Silva,  kutoka klabu ya Urussi Anzhi Makhachkala.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kutoka Brazilia alikuwa katika harakati za kusaini mkataba na Klaby ya Tottenham Hotspurs baada ya kufanya vipimo vya afya siku ya jumaatano ya wiliyopita.

 

Taarifa zaidi zinasema kuwa Chelsea walijitosa mnamo siku ya Alhamisi na kupendekeza kitita hicho na kufikia makubaliano na mchezaji huyo.

 

Mkataba huo umewezekana baada ya kuingilia kati kwa mmiliki wa Chelsea Roman

 

Abramovich, ambaye bepari mwenzake Mrussi Suleyman Kerimov anamiliki klabu ya Anzhi

Willian alitazamia kujiunga na Tottenham, lakini Chelsea ilipojitoa aliamua asikose fursa ya kucheza kwenye kombe la klabu bingwa ya Ulaya. Kwa mujibu wa duru za klabu hiyo Chelsea imekua ikimtafuta mchezaji huyo tangu  mwaka 2011.

 

Willian ni mchezaji wa tatu kusajiliwa Stamford Bridge baada ya Mjerumani Andre Schurrle na Marco van Ginkel wa Uholanzi.

 

 

 

By Jamhuri