Mchezaji wa kiungo wa kati wa Manchester City, Yaya Toure, ni kati ya wachezaji 23 waliotajwa kuwania tuzo ya mchezaji bora zaidi kwa mwaka huu wa tuzo za Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

Toure ni mchezaji pekee kutoka barani Afrika ambaye yumo katika orodha ya kuwani tuzo hiyo.

 

Katika tuzo hiyo FIFA imewajumuisha wachezaji wengine sita wa Klabu ya Bayern Munich kwenye orodha hiyo.

 

Jose Mourinho alitajwa kuwania tuzo ya kocha bora zaidi mwaka huu licha ya kushindwa kuiwezesha Klabu ya Real Madrid kutwaa taji lolote kubwa katika msimu uliopita.

 

Taarifa zinaonesha kuwa mchezaji pekee kutoka Uingereza ambaye aliteuliwa kuwania tuzo hiyo, Gareth Bale. Wachezaji wa Kimataifa kutoka Ujerumani ni Manuel Neuer, Bastian Schweinsteiger, Thomas Mueller na Phillip Lahm.

 

Wengine ni  Mfaransa Franck Ribery na Arjen Robben kutoka Uholanzi.

Wachezaji wengine maarufu walitajwa katika orodha hiyo ni Lionel Messi, Andres Ineasta na Cristiano Ronaldo.

 

Aliyekuwa Kocha wa Bayern Munchenun, Jupp Heynckes, ambaye nafasi yake imechukuliwa na Pep Guardiola naye ameteuliwa kuwania tuzo hiyo ya kuwa kocha bora zaidi baada ya kuongoza klabu yake kushinda Ligi ya Ujerumani (Bundesliga).

 

Guardiola ameiwezesha Bayern Munchenun kushinda Kombe la Ujerumani na Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.

 

Mshindi wa Tuzo ya Kocha Bora Afrika, Stephen Keshi kutoka Nigeria hakufanikiwa kuwa katika orodha hiyo.

 

1083 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!