Mpendwa msomaji,

 

Natumaini hujambo na unaendelea vyema. Kutokana na sababu zilizoko nje ya uwezo wetu, wavuti wetu haukuwa hewani kwa karibu miezi minne. Tumepigana kwa kila hali, tatizo hili limekwisha na sasa tunarejea hewani.

Tunaahidi kuendelea kuwatumikia kwa hali na mali. Nafurahi kuwajulisha kuwa tayari kampuni yetu sasa imetimiza miaka miwili tangu tumeianzisha pamoja na ‘ukapa’ unaovikabili vyombo vya habari, kwa ujumla nchini ila ninyi wasomaji wetu mmetuwezesha kuendelea kuwapo kwa nguvu kubwa.

Mungu awabariki sana na nawatakia ndugu zetu Waislamu kokote nchini na duniani mfungo mtukufu mwema.

Wenu,

 

Deodatus Balile,

Mhariri Mtendaji,

Jamhuri Media Limited

891 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!