*Barack Obama: Mweusi wa kwanza kuiongoza

* Kennedy: Ndiye Mkatoliki pekee kukubalika

*Franklin: Alidumu muda mrefu madarakani

*William Henry: Aliongoza kwa siku 32 pekee

Kwa mujibu wa Katiba ya Marekani, Rais wa Marekani ndiye mkuu wa nchi na Serikali ya Marekani. Ndiye mkuu wa Serikali ya Shirikisho, na ofisi ya rais ndiyo kubwa kiutawala nchini humo. Rais pia ndiye Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Marekani.

Rais anachaguliwa kuongoza kwa kipindi cha miaka minne. Mabadiliko ya Katiba ya Marekani ya mwaka 1951 yalizuia mtu mmoja kushika wadhifa wa Rais kwa vipindi zaidi ya viwili. Ikitokea Rais amefariki dunia, amepata maradhi, amejiuzulu au kuondolewa madarakani, Makamu wa Rais atashika wadhifa wa urais. Rais anatakiwa awe na umri walau wa miaka kuanzia 35, na awe Mmarekani wa kuzaliwa.

 

Marekani imekuwa marais 43 waliopa kushika wadhifa wa urais, lakini inajulikana kuwa Marekani imekuwa na marais 44 kwani Grover Cleveland alishika madaraka ya urais kwa vipindi viwili vilivyopishana na hivyo anatambulika kama rais wa 22 na wa 24 wa Marekani. Kati ya waliochaguliwa kushika wadhifa wa urais, wanne walifia ofisini kutokana na maradhi ya kawaida. Nao ni William Henry HarrisonZachary Taylor, “Warren G. Harding, na Franklin D. Roosevelt. Marais wanne waliuawa. Nao ni Abraham LincolnJames A. GarfieldWilliam McKinley, John F. Kennedy). Hadi sasa ni rais moja tu, Richard Nixon, aliyejiuzulu. George Washington, ambaye ni Rais wa Kwanza wa Marekani aliapishwa mwaka 1789 baada ya kupata ushindi mnono wa kura za majimbo (Electoral College). William Henry Harrison ndiye aliyekaa muda mfupi zaidi kwenye madaraka ya urais kwa siku 32 mnamo mwaka 1841.

 

Franklin D. Roosevelt ndiye aliyedumu madarakani kwa muda mrefu wa zaidi ya miaka 12. Alifariki dunia muda mfupi baada ya kuanza kuongoza awamu ya nne mwaka 1945. Ndiye rais pekee aliyeweza kuongoza kwa awamu zaidi ya mbili; na mabadiliko ya katiba yalizuia kuongoza zaidi ya vipindi viwili baada ya Harry Truman, kupitisha utaratibu wa ukomo wa mtu kuchaguliwa kuwa rais.

 

Andrew Jackson, ambaye ni rais wa awamu ya saba ndiye wa kwanza kuchaguliwa na watu wa kada zote mnamo mwaka 1828. Warren Harding ndiye rais wa kwanza kuchaguliwa baada ya kupitishwa kwa sheria iliyowaruhusu wanawake kupiga kura mwaka 1920.

 

Kumbukumbu zinaonesha kwamba marais John Q. Adams, Rutherford B. Hayes, Benjamin Harrison na George W. Bush, ambao walishindwa kwenye kura za wananchi (popular vote), lakini bado wanashika wadhifa huo. John F. Kennedy ndiye hadi sasa anayeshikilia rekodi ya kuwa rais wa Marekani ambaye ni muumini wa madhehebu ya Katoliki. Rais wa sasa, Barack Obama, ndiye rais wa kwanza wa Marekani mwenye asili ya Afrika.

1927 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!