Wiki iliyopita Waziri wa Sheria na Katiba,
Profesa Palamagamba Kabudi,

akiwa Marekani aliwapa darasa wana-
diaspora kuhusu mambo mazito ya historia

yetu na mambo yanayofanywa na serikali,
cha kushangaza kilichotiliwa mkazo ni swali
lililoulizwa kuhusu Tundu Lissu tu.
Watanzania tubadilike.
Msomaji wa JAMHURI, 0682874626

CCM iwe makini
CCM iwe makini, wale iliowaita mafisadi
wanarudi kiaina kwa kile wanachodai
kuridhishwa na utendaji wa awamu hii.
Kama ni kweli wayaseme hayo wakiwa
huko huko tu, nasi tutawaelewa.

Lusian Ngoromera, Morogoro, 0783473547

Mkandarasi anatukera
Barabara ya Kitunda kwenda Kivule
imetelekezwa na mkandarasi na
tunachoambulia wakazi wa maeneo haya ni
kupata maradhi ya kifua, hatuoni kazi
anayofanya mkandarasi huyu.
Msomaji wa JAMHURI, 0655677603

CCM imeoza
Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere,
aliwahi kusema CCM imeoza. Si vema
kuwanunua wapinzani, kuwapa vyeo na
kuwaacha Wana CCM halisi. Pia kutumia
Jeshi la Polisi na NEC kuchakachua kura za
wapinzani kwa kuibeba CCM na kutumia
vibaya mahakama.
Msomaji wa JAMHURI, Manyara,
0682880266

Ubabaishaji wa upinzani
Tunapenda kuona demokrasia ikianzia
ndani ya vyama, ikiwa ni pamoja na
ubadilishanaji wa madaraka, lakini viongozi

wao wapo tangu mfumo wa vyama vingi
uanze. Waachieni wengine.
Msomaji wa JAMHURI, Tanga, 0782205796

Hongera DC Tanga
Hakika tuna kiongozi bora mwenye kujua,
kutatua kero zetu na kumsikiliza kila
mwananchi katika Wilaya yetu ya Tanga
Mjini. Hongera Mkuu wa Wilaya, Mwilapwa,
Mungu akuzidishie katika utendaji kazi wako
pamoja na Rais wetu John Magufuli.
Msomaji wa JAMHURI, Tanga, 0656488227

Kodi na siasa
Bajeti ya nchi ambayo ni mgawanyo wa kodi
za wananchi ina uhusiano gani na mbunge?
Mimi hata kura sipigi, sina chama,
mnanichanganya mnapohusisha kodi yangu
na siasa zenu. Utasikia ukimchagua huyu
hatutaleta hiki au kile.
Kapaya Kapaya, 0752659991

Tiketi ya bodaboda
Huwezi kuamini, hakimu wa Mahakama ya
Mwanzo Kenyana, Wilaya ya Serengeti

anamwomba mlalamikaji tiketi ya bodaboda.
Huu ni ukiukaji wa maadili ya kimahakama
na kupindisha sheria, mahakimu wa namna
hii hawafai kabisa wala hawatoa haki kwa
wanyonge.
Waziri husika upo?
Revocatus Machage, Ngoreme, Musoma,
0759030344

Bodaboda mjini
Waziri Kangi Lugola ruhusu pikipiki tupeleke
abiria mjini ambako tunakatazwa, lakini
wakubwa wamejaza pikipiki zao tena
hawavai hata kofia ngumu.
Msomaji wa JAMHURI, Dar es Salaam,
0655617153

Isenegeja turudishiwe ardhi
Wananchi wa Isenegeja, Igunga,
hatutendewi haki na watendaji wa vijiji.
Tunadai shamba lililoporwa na Mwalimu
Mkuu wa Shule ya Isenegeja na Kamati ya
Serikali ya Kijiji ilifanya kikao na kuturuhusu
tuendelee kulima mashamba hayo baada ya
kutatua tatizo lakini bado tatizo linaendelea
hadi sasa. Tunaomba serikali itusaidie.

Msomaji wa JAMHURI, 0782701712

Ushuru wa daladala
Ni nani anayehusika na usimamizi wa vituo
vya daladala hapa Dar es Salaam? Vituo
vimechakaa kweli na ushuru unatolewa kila
siku. Tunaomba ukarabati wa vituo hivi
ufanyike.
Msomaji wa JAMHURI, 0623444737

JAMHURI liboreshwe
Mhariri, mimi ni msomaji mzuri sana wa
Gazeti lako la JAMHURI na liliwahi kusifiwa
na rais. Sasa naona uzuri wa taswira hiyo
umeanza kupotea kwa wengine kuandika
masuala ya kitaaluma, naomba waige
mfano wa Mpendu, Zuzu, Dk. Kamugisha
na mzee Mbena, si kila toleo mambo
yaleyale tu.
Lusian Ngoromera, Morogoro, 0659651575

Vyama vya upinzani
Nawashauri Watanzania wenzangu, hakuna
nchi iliyoendelea bila upinzani; na wote
walioacha uongozi Chadema, CUF na
kukimbilia CCM wamerubuniwa tu. Upinzani

ni wa muhimu sana, na kama si wa
muhimu, ni mpinzani yupi amewahi
kukamatwa kwa kuhujumu mali ya umma?
Msomaji wa JAMHURI, 0768196095

Umeme wa REA
Umeme wa REA awamu ya pili na tatu uko
wapi? Tangu awamu ya kwanza maeneo ya
Ngoreme, Wilaya ya Serengeti hatujaona
tena dalili za awamu ya pili na ya tatu, licha
ya baadhi ya taasisi kuwa jirani na ‘line’ kuu
ya umeme.
Msomaji wa JAMHURI, 0763444011

Wizara ya Elimu
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi iangalie tatizo kubwa la kufanya
vibaya wanafunzi katika mitihani yao ya
mwisho ya kumaliza elimu ya msingi na
sekondari. Tumeona kila mwaka kiwango
cha ufaulu kwa wanafunzi wa shule za kata
ni kidogo.
Salim Liundi, Mtoni, Dar es Salaam,
0763036009

Utapeli Muheza
Huku kwetu Muheza, Tanga fedha
zinazotolewa kwa ajili ya kuwasaidia
maskini na wazee asilimia kubwa wanapata
vijana ambao si walengwa. Naomba serikali
iangalie hilo.
Mariamu Peter, Muheza, Tanga,
0656600932

Wabunge njaa tupu
Nimeshuhudia huko nyuma watu wakiacha
kazi zenye mshahara mnono mfano; BoT,
TRA n.k. wakikimbilia ubunge, lakini kwa
sasa watu wanauacha ubunge na kuamua
kukaa mitaani kumuunga mkono JPM.
Msomaji wa JAMHURI, 0767633526

Hongera Simba
Hongera sana wachezaji wa Timu ya Simba
kwa mchezo mzuri dhidi ya Ndanda FC,
hakika nimeiona bidii yenu ila kila mchezo
una aina ya wachezaji wanaostahili
kupangwa kutokana na mazingira kwa
mechi za mikoani.

Samora John, Askona, Karatu, 0717479457

Makocha Simba
Uongozi Simba umalize tofauti na makocha,
vinginevyo ubingwa hakuna msimu huu.
Samora John, Askona, Karatu, 0717479457

Lukuvi uje Kigoma
Baraza la Ardhi na Nyumba Mkoa wa
Kigoma ni tatizo, kesi zinapigwa kalenda tu
na matokeo yake watu wanakata tamaa.
Kesi hutoka wilaya zote za Mkoa wa
Kigoma, Waziri Lukuvi, njoo uone kuna
tatizo gani au wenyeviti hawatoshi?
Msomaji wa JAMHURI, 0762315456

Wapiga debe
Wapiga debe na makondakta wa daladala
Dar es Salaam acheni uhuni.
Wanawalazimisha abiria kupanda magari na
wanapokataa wanawafanyia fujo,
kuwaporomoshea matusi ya nguoni na

kuwatishia maisha. Polisi ondoeni kero hii
kwa wananchi katika vituo vyote vya
daladala hasa Mwenge, Morocco, Tegeta,
Nyuki na Bunju Mwisho.
Msomaji wa JAMHURI, 0789783789

Watanzania tuelimike
Sifurahishwi na tabia za baadhi ya watu
ambao wamekuwa na mtindo wa kubipu
simu za jamaa zao ili wapigiwe wakati wao
ndio wenye shida. Tabia hiyo si nzuri kwa
sababu unaweza kuwa na shida za muhimu
watu wakashindwa kukusaidia. Isitoshe
kampuni za simu zimepunguza gharama.
Salim Liundi, Mtoni kwa Azizi Ally, Dar es
Salaam, 0659601205

Rushwa
Kabla ya yote nampongeza Rais John
Magufuli kwa kupambana na rushwa na
ufisadi kadiri ya uwezo wake. Ameinyoshea
kidole Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (TAKUKURU), sitaenda mbali na
ukweli kuwa hamahama ya wapinzani ina

harufu ya rushwa. Rushwa na ufisadi
havitakoma.
Msomaji wa JAMHURI, Usagara, Mwanza,
0682880266

Brigedia Mbenna
Baada ya kutafakari makala ‘Asili ya vyama
vya siasa’ katika Gazeti la JAMHURI,
Mwandishi Brigedia Mbenna anapandikiza
chuki katika mfumo wa vyama vya upinzani
kwa enzi zilizopitwa na wakati za kina Adolf
Hitler (Mjerumani) na Paul Krugger wa
Afrika Kusini enzi za makaburu. Ya kale
yamepita, tugange yajayo.
Msomaji wa JAMHURI, Mwanza,
0682880266

Wafugaji Serengeti
Rais Magufuli ni ukweli usiopingika kuwa
ziara yako mkoani Mara imeleta faraja
katika nyanja mbalimbali lakini umeisahau
mifugo yetu sisi wafugaji, kwani haina maji
ya uhakika. Tunakuomba walau tujengewe
marambo mawili kila kata hapa Ngoreme,
Serengeti, Mara.

Revocatus Machage, Serengeti, Mara,
0759030344

Ajira
Vijana wapewe mafunzo ya uzalishaji mali,
ufundi, kilimo, biashara na ujasiriamali ili
kujiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa.
Omari Ramadhani, 0655225339

Viwanda
Ujenzi wa viwanda ufuatane na upatikanaji
wa malighafi katika eneo husika.
Msomaji wa JAMHURI, 0655225339

Utunzaji mazingira
Utunzaji na uhifadhi wa mazingira ya bahari,
mito, maziwa visima, ardhi oevu viwekewe
sera, sheria, miongozo na mikakati ya
kuvitunza ili visaidie vizazi vya sasa na
vijavyo.
Omari Ramadhani, 0655225339

Mwisho

844 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!