Waziri wa Elimu, Prof. Joyce Ndalichako amewaagiza Wakurugenzi wa Elimu kuhakikisha kuwa, wanafunzi wote waliofukuzwa shule kutokana na kushindwa kutoa michango mbalimbali warudishwe mara moja na wazazi waliotoa michango yao warudishiwe.

Ameyasama hayo leo baada kupokea agizo kutoka kwa Rais Magufuli akiwataka kwenda kuwaagiza wakuu wilaya, Wakurugenzi kuhakikisha hakutakuwa na mwanafunzi anayefukuzwa shule kutokana kushindwa kulipia michango ya shule na amesema atakayeshindwa kusimamia hilo basi kama amemteua hatashindwa kumfukuza kazi.

Rais Magufuli amesema yeye hajakataza michango ambayo huwa wanakubaliana kati ya wazazi na kamati ya shule ila isiyokigezo cha kuwafukuza wanafunzi shule.

1428 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!