Kufuatia matokeo ya jana kuanzia mchezo wa mapema uliowakutanisha Simba na URA, na kushuhudia Simba kipandishwa boti kurudi Dar es Salaam kwa kufungwa bao 1-0, na kuifanya URA kufika point 10 na kuongoza kundi A huku Azam ikishika nafasi ya pili kwa kufikisha Point 9.

Yanga nao wemeshindwa kuwafunga Singida United baada ya kutoka nayo sare kwa kufungana bao 1-1, Matokeo hayo yanaifanya Singida United kuwa vinara wa kundi B, kwa kufikisha pointi 13 sawa na Yanga lakini yenyewe inawastni mzuri wa mabao ya kufunga tofauti na Yanga ambayo inamabao machache.

Singida United itacheza na Azam FC ilishika nafasi ya pili kwenye kundi A, Jumatano usiku wakati siku hiyo hiyo Yanga itamenyana na URA ya Uganda katika mchezo wa nusu fainali ya kwanza ambayo imepangwa kupigwa kuanzia majira ya saa 10:30 slasiri.

By Jamhuri