Kocha wa Yanga amesema hawatotumia mchezaji mwingine zaidi ya wale waliokuwa wakiwatumia tangu mwanzoni mwa michuano hiyo

YANGA na URA zitashuka dimbani mapema kesho kutafuta timu itakayocheza fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi ambalo linaendelea hapa visiwani Zanizibar

Mchezo huo unatarajiwa kuanza majira ya saa 10:30, na unatarajiwa kuwa na presha kubwa kwa pande zote mbili hasa wenyeji Yanga ambao watakuwa na kazi ya kukwepa aibu baada ya URA kuzifunga timu mbili kubwa nchini za Azam FC na Simba kwenye mechi za hatua ya makundi.

Yanga ambayo mashabiki hawaipi nafasi kubwa ya kutinga fainali kutokana na ubora wa kikosi cha URA, imefik hatua hiyo baada ya kumaliza ya pili kwenye Kundi B, ikiwa na pointi 13, katika mechi tano ilizocheza ambapo ilishinda nne na kutoka sare mchezo mmoja na imefunga mbao saba na kufungwa mawili wakati URA wamefika hatua hiyo kwa kumaliza nafasi ya kwanza kwenye kundi A wakijikusanyia pointi 10 mabao manne ya kufunga na kufungwa moja  katika michezo minne waliyocheza.

Takwimu hizo zinaonyesha namna safu ya ushambuliaji ya Yanga ilivyokuwa kali lakini pia inaonyesha ni namna gani ulinzi wa URA ulivyokuwa makini kwa kuruhusu bao moja tena dhidi ya timu ngumu za Azam FC nA Simba waliokuwa nao kundi moja.

Kocha msaidizi wa Yanga amekiri kuwa wapinzani wao URA, ni timu nzuri na ngumu, lakini akahidi hawato waogopa watacheza kwa ari ileile
waliyoitumia kwenye mechi za makundi na kuhakikisha wanatinga fainali.

“URA ni wazuri wameifunga Azam pamoja na Simba, tumewaona uchezaji wao lakini nasisi tutajipanga kuitumia vizuri siku moja ya mapumziko ili
tuweze kujipanga na kushinda mchezo huo kama ambavyo tumekusudia,” amesema Nsajigwa.

Kocha huyo amesema hawana mpango wa kuongeza mchezaji mwingine yeyote kwenye kikosi chao kuelekea mchezo huo kwani wanawaamini wachezaji
waliopo na ndiyo wataendelea kuwapa nafasi hadi mwisho ya michuano hiyo bila kujali wanakwenda kucheza na timu gani.

Katika mchezo huo kiungo Papy Kabamba Tshishimbi anatarajiwa kurudi uwanjani baada ya kuukosa mchezo dhidi ya Singida United, na Nsajigwa
alisema wataendelea kutumia mfumo uleule wa kucheza kwa kushambulia nwote na kurudi kukaba kwasababu anajua URA inawachezaji wenye nguvu
na kutumia sana mashambulizi ya kustukiza (Count Attack).

Kwaupande wake kocha wa URA, Nkata Paul, amesema wa leo utakuwa mgumu kwao kutokana na staili inayotumiwa na wapinzani wao Yanga, ambayo ni
vigumu kuwadhibiti hasa wanapokwenda kushambulia.

Nkata alitolea mfano juhu zilizoonyeshwa na wachezaji wa Yanga katika mchezo wao wa mwisho wa makundi dhidi ya Singida United na kusawazisha
bao dakika ya mwisho jambo hilo limempa hofu na kusema kuwa anakazi ya kufanya.

Kocha huyo anajivunia ubora wa kipa wake Alionzi Nafian ambaye alionyesha uwezo mkubwa katika mchezo dhidi ya Simba pamoja na safu
yake ya ushambuliaji ambayo imekuwa na maelewano mazuri tangu kuanza kwa michuano hiyo.

Uwepo wa washambuliaji Sseruyide Moses, Shafiq Kagimu, Kalama Deboss na Kagaba Nicholas, kunaweza kuondosha ndoto za Yanga kucheza fainali
endapo safu yake ya ulinzi haitokuwa makini kuwadhibiti wachezaji haoambao wameonekana ni hatari wanapokuwa kwenye uso wa lango la timu pinzani.

By Jamhuri