Bodi ya ligi (TPLB) imetangaza maboresho katika zawadi za mchezaji bora wa mwezi wa Ligi kuu Tanzania Bara, ambapo kuanzia sasa, mchezaji bora wa kila mwezi atakuwa akipata tuzo maalum ya Kikombe, fedha taslim shilingi milioni moja pamoja na king’amuzi cha Azam TV.

Afisa Mtendaji Mkuu wa bodi hiyo, Boniface Wambura amesema zawadi zilizoongezwa ni tuzo itakayokuwa ikitolewa na bodi hiyo pamoja na king’amuzi ambacho kitakuwa kikitolewa na Azam TV kama wadhamini wa ligi hiyo upande wa matangazo ya televisheni, huku shilingi milioni moja iliyokuwepo tangu awali, ikiendelea kutolewa na wadhamini wakuu wa ligi hiyo Kampuni ya simu za Mikononi ya Vodacom.

Wambura Ameongeza  tayari zawadi hizo mpya zimeanza kutolewa kwa aliyekuwa mchezaji bora wa mwezi Novemba, Mudhathir Yahya wa Singida United na kesho (Januari 11, 2018) mchezaji bora wa mwezi Desmba 2017 anatarajia kutangazwa.

By Jamhuri