Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe leo ameweka taarifa za mali zake zote zikiwemo, madeni anayodaiwa, mshahara na mali alizonazo kwa mwaka 2016, kama sheria inavyoagiza viongozi wa umma.

Zitto pia ametoa rai kuwa ni vyema Daftari la Rasilimali na Madeni la Viongozi wa Umma likawekwa wazi mitandaoni kwa ajili ya umma ili kufahamu kila mtu anamiliki mali alizo nazo kwa njia gani.

Mbali na Zitto Kabwe kuwasilisha mali zake pia Rais Magufuli ameshawasilisha mali zake na amemtaka Kamishna wa Maadili, Jaji Mstaafu, Harold Nsekela kutopokea fomu ya kiongozi yoyote ambaye atakuwa hajawasilisha tamko lake la mali na madeni ifikapo Disemba 31, 2017.

2753 Total Views 2 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!