Zuma Agoma Kung’atuka Madarakani

South African President Jacob Zuma in the capital, Pretoria, August 19, 2017.

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amekataa wito wa chama chake wa kujiuzulu kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo.

Rais huyo amekuwa anakabiliwa na shinikizo zaidi kujiuzulu kufuatia mazungumzo na maafisa wa ngazi ya juu katika chama chake cha ANC siku ya Jumapili.

Haijafichuliwa mazungumzo hayo yalihusu nini .

Bw Zuma aliyefungwa gerezani baada ya kuhsiriki katika vita dhidi ya ubaguzi wa rangi anaonekana kuwa katika hatua za mwisho wa awamu wake wa pili na wa mwisho kama Rais.

Julius Malema, kiongozi wa upinzani na aliyekuwa mafuasi wa chama hicho cha ANC alisema kwenye mtandao wake wa Twitter kwamba rais Zuma amekataa kujiuzulu.

Habari ambazo hazijathibitiwa zinasema kuwa katika mkutano wa Jumapili Zuma aliomba kupata kinga dhidi ya kushtakiwa kwa yeye na familia yake.

Cyril Ramaphosa aliichukuwa nafasi ya kiongozi wa chama cha ANC kutoka kwa Zuma, anayekabiliwa na tuhuma za rushwa.

Wachambuzi wanasema wakuu wa chama hicho wanajaribu kuondoa mvutano wa kung’ang’ania madaraka ambao unaweza kukigawanya chama hicho kabla ya uchaguzi mkuu mwakani.

Wanatarajiwa kuanza mchakato wa kumuondoa rais Zuma kupitia mfumo rasmi wa kumuondoa au kwa kuidhinisha hoja bungeni.

Maafisa sita wakuu wa chama hicho tawala waliwasili mmoja baada ya mwingine Jumapili katika makaaziya Zuma mjini Pretoria.

Walinyamaza kimya wakati mazungumzo yalipomalizika lakini wameitisha mkutano wa kamati kuu ya chama hicho Jumatatu.

Zuma anastahili kusalia madarakani hadi uchaguzi mwaka ujao 2019. Hatahivyo chama hicho kimepoteza umaarufu wake katika muhula wa pili wa kiongozi huyo huku kukishuhudiwa pia kudorora kwa uchumi na tuhuma za rushwa.