Jeshi la Polisi Mkoa Wa Tanga limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 94 kwa makosa mbalimbali ikiwemo uvunjaji ,mauaji,kujeruhi ,kusafirisha wahamiaji haramu ,kuharibu mali pamoja na kupatikana na silaha sita aina ya Gobole.

Akiongea na waandishi wa habari kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi wakati akitoa taarifa ya oparesheni mbalimbali zilizofanywa na Jeshi hilo katika kipindi Cha mwezi mmoja .

Amesema katika kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya wamefanikiwa kukamata wasafirishaji wa dawa za kulevya aina ya mirungi na wauzaji wa dawa za kulevya aina ya bangi ambao ni Godwin Nemes (23)  mkazi wa Rombo Kilimanjaro akiwa na mwezake Christopher John (18)  mkazi wa Rombo ambapo kilo 307.5 za mirungu na kilogramu 73 za bangi zimekamatwa.