Wenye kalamu, makaratasi huu ndio wakati wenu kwakuwa wapiga picha wao washamaliza kazi yao, yaani kaeni tayari sasa kuandika historia mpya kutoka hapa wilayani Karatu mkoani Arusha ambapo nyomi hili la wananchi hawa limejitokeza wakiwa na shangwe kwelikweli huku wakisema wametoka nyumbani kuja kumpokea na kumsikiliza Mgombea wa Urais kupitia CCM, Rais Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻 leo tarehe 3 Oktoba 2025.
Dkt. Samia atanadi ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025/30 , sera na ahadi zake ikiwa ni pamoja na kuomba kura za ndiyo kwa mafiga yote matatu yaani Rais , Wabunge na Madiwani.
Huu ni muendelezo wa mikutano ya kampeni za Urais kupitia CCM ndani ya mkoa wa Arusha ambapo baada ya hapa, Dkt. Samia anatarjiwa kupokelewa kwa kishindo ndani ya mkoa wa Manyara.









