Mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wakazi wa Dar es Salaam kuwa kuanzia Januari mwaka ujao wataanza kuona mageuzi makubwa ya uendeshaji wa mabasi ya mwendokasi (BRT).


Rais Samia ametoa kauli hiyo wakati wa mkutano wake wa kampeni za uchaguzi mkuu ziliozofanyika viwanja vya Leaders, Kinondoni jijini Dar es Salaam leo Oktoba 21,2025.

Tumejenga miundombinu ya barabara yenye umbali wa kilomita 95, ambapo kipindi hiki jumla shilingi trilioni 2.1 zimetumika, tunapokwenda mbele ujenzi wa awamu zote za miradi tunakwenda kuzisimamia na kuzimaliza.

Tutasimamia uamuzi wetu wa kushirikisha zaidi sekta binafsi, tutakapomaliza baraabara zote ni fursa muhimu kwa sekta hii kupata kazi ya kubeba abiria na kurudisha. Kazi hii kwa kiasi kikubwa hatutaki kuifanya serikali, bali sekta binfasi wataingiza mabasi yao kwa ajili ya kuendesha shughuli hizi,amesema.

Amesema tayari mpaka sasa serikali imepata watoa huduma kwenye awamu ya kwanza ambapo makampuni mbalimbali na idadi ya mabasi kwenye mabano kuwa ni ENG (77), Mofat (255), YG Link (166) na Metro Link City (334).

Makampuni haya yote niliyotaja yataingia kutoa huduma, japo yapo mengi tayari yameanza kutoa huduma huko barabarani, ahadi yetu kwenu ni kuwa kuanzia Januari, mwakani wakazi wa Dar es Salaam mtaanza kuona mageuzi makubwa kwenye utoaji wa huduma kwenye barabara za BRT.

Nataka niwambie mradi huu hata hatua hii tuliyofikia imetujengea sifa kimataifa, Tanzania tayari una sifa kimataifa katika uwekezaji wa katika jiji letu la Dar es Salaam.

Nihawakikishie wakazi wa Ubungo, Kinondoni na Dar es Salaam kwa ujumla kuwa kwa mageuzi yaliyofanyika kwenye uendeshaji kuwa tutalinda sifa hiyo kwa sababu BRT italeta mapinduzi makubwa kwenye usafiri,amesema.


Kuhusu daladala zinazotoa huduma pembezoni mwa jiji hilo, Rais Samia amesema serikali itachukua hatua kadhaa za maboresho ya stendi.

“Kipindi hiki tumekamilisha ujenzi wa stendi ya Mwenge, tunapokwenda tunakwenda kufanya ukarabati ili kuzibiresho stendi za Kawe, Bunju B na Tegata Nyuki ili ziwe na maeneo maalumu na kuzipangia ruti maalumu za kutoa huduma za daladala.

Pamoja na kusimamia ukuaji mzuri wa uchumi wetu, hapa nazungumzia uwezeshaji wananchi kiuchumi, wafanyabiashara ndogo ndogo mambo ya masoko na stendi. Nataka wana Dar es Salaam tuvute ramani, tuanze maeneo ya Mbuyuni njia ya kwenda Moroco piga picha iliyokuwapo ya vibanda vya plastiki za rangi mbalimbali zinateremka mpaka Mwenge, vikasogea karibu na Lugalo wakaheshimu pale jeshini tu, miaka saba iliyopita. Sasa havipo aliyekuja kuja akashukia katikati ya jiji sasa havipo. Jiji sasa linangara na mji unaotambulika.amesema.

Amesema kuondoa vibanda ni hatua moja, lakini kuwawezesha wenye vibanda kupata maeneo ya kufanyia biashatra au kupata mitaji ni jambo jingine.

Amesema uchumi wa Tanzania umepanda kwa asilimia 5.5, kutoka asilimia 4 wakati wanapokea uongozi wa nchi mwaka 2021.

Tumechukua hatua mbalimbali kuboresha mazingira kwa wafanyabiashara na wajasiriamali, Kinondoni tumejenga masoko ya Tandare, Magomeni na Bwawani, kwa Ubungo tumejenga mradi wa uwekezaji katika soko la Manzese, tumeboresha soko la Simu 2000, Mbezi Luis na Mbezi njia ya kwenda Goba, miradi hii imeboresha maisha ya wafanyabaishara,amesema.


Kuhusu wafanyabiashara wa Kawe, Rais Samia ameahidi kujenga soko jipya la kisasa litakalowezesha kufanya biashara kwa usalama na ubira unaotakiwa.