Na Heri Shaaban, JamhuriMedia, IIala

MKUU wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, amewataka Madiwani wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam, kufanya kazi kwa kushirikiana na Watendaji na Wenyeviti wa Serikali za mitaa katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi

Mkuu wa Wilaya Edward Mpogolo, alisema hayo wilayani Ilala ,wakati wa kufunga mafunzo ya siku tatu ya madiwani wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam yaliokuwa yakiwajengea uwezo.

“Nawaomba madiwani wangu wa Halmashauri ya jiji mkawe kiunganishi baina yenu na Watendaji pamoja na Wenyeviti wa Serikali za mitaa katika kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi ili tumsaidie Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassan “alisema Mpogolo.

Mpogolo aliwataka madiwani kushuka chini ngazi ya Mtaa kwa kushirikiana na Watendaji na Wenyeviti ndio kwenye kero kubwa ikiwemo kuweka vikao vya utatuzi wa kero na mikutano ya wananchi

Mkuu wa Wilaya Edward Mpogolo alisema mafunzo hayo yawe na tija kwa ajili ya kuwatumikia wananchi katika maeneo yao .

Alisema ukijua shida za watu uwezi kuona mzigo kuhudumia aliwataka waende kutatua kero za wananchi katika kata zao ,mitaa yao na maeneo yao.

Aidha alisema dhumuni la mafunzo hayo kuwajengea uwezo madiwani juu ya uwendeshaji Mamlaka za Serikali za mitaa .

Wakati huo huo amewataka Madiwani Ilala kwenda kusimamia ukusanyaji mapato ya Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam ili Serikali iweze kufikia malengo katika kukusanya mapato mengi .

Kwa upande mwingine aliwataka madiwani wa Halmashauri kwenda kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali kuu.