Na Heri Shaaban, Dar es Salaam
MKUU wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, amesema Wilaya ya Ilala, wanafanya kazi kwa umoja na mshikamano Watendaji wa Halmashauri hiyo pamoja na Wabunge wa vyama vyote siasa katika kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kutatua kero za wananchi.
Mkuu wa Wilaya Edward Mpogolo, alisema hayo kata ya Zingiziwa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam wakati wa ziara ya pamoja madiwani wa jimbo la Ukonga pamoja na Wabunge wa Jimbo la Ukonga Bakari Shingo (ACT Wazalendo)na Mbunge wa Jimbo la Kivule Ojambi Didas Masaburi (CCM) katika tukio lililoandaliwa na Diwani wa Zingiziwa Selemani Kaniki, kukabidhi nyumba kwa Mama Mjane Fatuma Msham .

“Tumekuja Zingiziwa kwa ajili ya dhamira ya kumuunga mkono Diwani Selemani Kaniki ,amefanya mambo makubwa kuisaidia Jamii ni Diwani wa kwanza kufanya jambo kubwa kama ili kumjengea nyumba mama Mjane Fatuma Msham Serikali inakupongeza sana kwa kuigusa jamii moja kwa moja “alisema Mpogolo
“Wilaya ya Ilala tunafanya kazi kwa umoja na mshikamano ni ishara njema Wilaya ya Ilala iko salama Wabunge wote tunashirikiana nao kazi pamoja yote ni kuisaidia Serikali ya Dkt.Samia Suluhu Hassan”alisema
Alisema tukio aliyofanya Diwani wa Zingiziwa Selemani Kaniki sawa na mfano Mwalimu Julius Nyerere aliweza kumjengea nyumba Mzee Maganga, na kumpa chakula zote hizi ni sehemu ya sifa ya Kiongozi Selemani Kaniki.
Aidha Mpogolo alisema Selemani Kaniki angeweza kujenga shule hospitali lakini mwananchi huyo shida yake ilikuwa nyumba na Serikali itasaidia ambapo katika jambo hilo ameonyesha sawabu kubwa sana.
Alisema katika changamoto zipo nyingi kila sehemu katika shida tuwashirikishe watu waweze kuwasaidia.

Wakati huo huo alisema Serikali imetoa vifaa vya kisima kuhakikisha kila jimbo linachimba visima vya maji ya DAWASA kwa ajili ya kumtua ndoo kichwani mama kuwaondolea adha ya maji ambapo aliwataka madiwani,Wenyeviti na Wabunge kushirikiana pamoja kutumikia wananchi na kuendeleza Amani na umoja.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga Bakari Shingo, aliguswa katika tukio la Mjane Fatuma Msham alichangia shilingi 500,000/= pamoja na thamani ya nyumba hiyo ikiwemo kuweka Talizi.
Akizungumza katika ufunguzi wa nyumba ya Mjane Fatuma Msham Selemani Kaniki alisema awali nyumba hiyo ilikuwa ya Matope alipokea kero hiyo ya kumsaidia kujenga kwa sasa nyumba ya kisasa imekamilika kwa ajili ya kuishi sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi CCM Kazi na Utu.





