Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Wananchi nchini wameshauriwa ,kutumia kinywaji chenye radha asilia cha Vin Nko kinachopatikana kwa baadhi ya nchi.

Hayo yamebaiisha na Mkurugenzi wa Kampuni ya Cavido Company Limited Dominick Salamba wakati wa uzinduzi wa kinywaji hicho cha Vin Nkolo Mboka chenye radha asilia kutoka Kampuni ya Simba Beverage Limited (SBL)

Salamba amesema ujio wa kampuni hiyo nchini, ni mojaya mapinduzi katika sekta ya vinywaji na kufungua fursa za ajira.

Amesema kampuni yao kwa kushirikiana na SBL wameamua kuwaletea Watanzania kinywaji chenye radha ya kipekee kinachotumia viungo vya asili ili kuwapa walaji ladha tofauti na yenye manufaa kiafya.

“Ujio wa kampuni yetu utaleta mapinduzi katika utengenezaji wa vinywaji,kwa muda mrefu wamekuwa wakifanya kazi katika nchi za Magharibi, lakini mwaka huu wameamua kuingia rasmi katika soko la Tanzania,” amesema.

Kwa mujibu wa maelezo yake, kinywaji kilichoanza kuzalishwa kinajulikana kama Vin Nkolomboka, ambacho kimetengenezwa kwa mchanganyiko wa viungo asilia ikiwemo Asali, Pilipili Manga na Tangawizi, kwa lengo la kuboresha radha pamoja na kusaidia afya na nguvu za mtumiaji wakati wa utendaji wa kazi.

Amesisitiza kuwa bidhaa hiyo ni ya kipekee kwani hakuna kampuni nyingine nchini inayozalisha kinywaji cha aina hiyo kwa kutumia mchanganyiko huo wa viungo asilia, tofauti na vinywaji vingi kama
vilivyozoeleka,

Aidha, kampuni hizo zimesema zitatumia vyombo vya habari kuufahamisha umma kuhusu ujio wa kinywaji hicho ambacho kimeelezwa kuwa hakina madhara na kinatarajiwa kuanza kupatikana sokoni muda si mrefu.

“Vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika kuwafikia wananchi, hivyo tutaendelea kushirikiana navyo katika hatua zote za utangazaji wa bidhaa hii na nyingine zitakazofuata,” aliongeza.

Uzinduzi huo unaelezwa kuwa ni mwanzo wa kampeni pana ya kutambulisha bidhaa mpya za vinywaji asilia katika soko la Tanzania.