Wadau mbalimbali wa sekta ya Afya wilayani Bunda, wamesema wako tayari kushirikiana na TAKUKURU kudhibiti mianya ya rushwa katika utoaji wa huduma za afya pindi wanapotumia mifumo ya kielektroniki ya utoaji huduma hizo.

Ahadi hiyo imetolewa katika warsha iliyoandaliwa na TAKUKURU iliyohusu Udhibiti wa Mianya ya Rushwa katika Mifumo ya Utoaji Huduma za Afya inayotumiwa na Hospitali Teule ya Wilaya ya Bunda.

Warsha hii imefanyika katika ukumbi wa Balili Rock Resort – Bunda, ambapo majadiliano yaliongozwa na Bw. Marko Machele – Katibu Mkuu wa Kanisa la Kilutheri Tanzania (K.K.K.T) Dayosisi Mkoani Mara.

Akiongoza mjadala huo Bw. Machelle alisema vituo vya kutolea huduma za afya vinalenga kutoa huduma bora kwa wananchi na ili huduma hizo ziwe bora ni lazima kudhibiti vitendo vya rushwa itakayowezesha kupata mapato ya kutosha.