Marekani imesifu operesheni yake nchini Iran na kusema inaelekea kumuangamiza adui hata kabla ya wakati huku ikisisitiza kuwa uwezo wa mashambulizi wa Iran umepungua maradufu ukilinganisha na siku ya kwanza ya vita.

Kamanda mkuu wa Jeshi la Marekani Brad Cooper, amesema mashambulizi ya Iran iwe ya makombora ya masafa marefu au droni yamepungua maradufu ukilinganisha na siku ya kwanza ya mzozo huo wa  Mashariki ya Kati , lakini akasisitiza kuwa wataendelea kuwa makini wakati wote.

Ama Rais wa Marekani Donald Trump kwa upande wake amesifu ufanisi wa operesheni hiyo akisema kuwa jeshi la Marekani, pamoja na washirika wazuri wa Israel, linaendelea kumuangamiza kabisa adui ambaye ni Iran, hata kabla ya muda uliopangwa.

” Pia tunawasihi wanadiplomasia wa Iran kote ulimwenguni kuomba hifadhi na kutusaidia kuijenga Iran mpya, iliyo bora na yenye uwezo mkubwa. Nadhani sasa unaanza mustakabali mzuri zaidi kwa Iran. Na Marekani itahakikisha kwamba kiongozi ajaye wa Iran hatatishia Marekani, Israel, majirani zake au mtu yeyote,” alisisitiza Trump.