Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa Africa50 ,ambapo Rais Samia Suluhu Hassan anatafungua mkutano huo kama mwenyejji na mwenyekiti.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za wizara hiyo Waziri wa fedha Balozi Khamis Musa Omari amesema mkutano huo, unatarajiwa, kuhudhuliwa na zaidi ya washiriki 1200 kutoka Afrika na duniani wakiwemo viongozi na wadau kutoka taasisi mbalimbali za serikali ,sekta binafsi na wadau wa maendeleo kutoka Afrika.

Amesema mkutano huo ,unatarajiwa kuchochea biashara na utalii ,ubia kati ya sekta za umma na sekta binafsi pamoja na kuimarisha mahusiano ya kiuchumi kati ya Tanzania na mataifa mbalimbali.

Amesema mkutano huo unafanyika wakati ambapo Afrika50 inatimiza miaka kumi tangu ilipoanza rasmi shughuli zake mwaka 2016 kwa ushirikiano wa serikali za Afrika na benki ya maendeleo ya Afrika AFDB

Kufuatia uamuzi wa wakuu wa nchi za Afrika ,kwa ajili ya kurahisisha utekekelezaji wa miradi ya kimkakati ya miundo mbinu ,ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa dira ya umoja wa Afrika.

Amesema mkutano huo ni wa siku mbili tarehe 5 na 6 ,ambapo , shughuli zitakazofanyika ni pamoja na mkutano mkuu , hafla ya kusaini makunaliano mbalimbali ya maandalizi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya miundo mbinu.