Mussa Juma,Meatu
Taasisi ya Friedkin Conservation Fund(FCF),imeanza majaribio ya matumizi ya Mizinga ya Nyuki ya Plastiki ambayo ni rafiki kwa mazingira na itagawanywa katika vikundi vya ufugaji Nyuki wilaya ya Meatu,Mkoa wa Simiyu.
Mizinga hiyo pia inatarajiwa kuongeza uzalishaji wa Asali mara tatu zaidi ya mizinga ya sasa ambayo hutengenezwa kwa mbao, miti na mabati.
Akiwasilisha taarifa ya Friedkin na Mwiba Holdings LTD ya miradi ya Uwezeshaji na Maendeleo ya Jamii
katika Jukwaa la Mashirika yasiyo ya Serikali (AZAKI) Wilaya ya Meatu Afisa mafunzo ya Ufugaji Nyuki wa FCF
Baraka Mabula anasema tayari Makundi ya Nyuki yameanza kutumia baadhi ya mizinga hiyo.
Mabula anasema technolojia ya Mizinga hiyo ambayo imetoka nchini Uturuki,itasaidia kuzuia utaratibu wa uchomaji moto katika uvunaji asali lakini pia mfugaji kwa mwaka mmoja atalina asali mara tatu.
Anasema mizinga hiyo inamfumo wa kudhibiti joto kali,tayari ina masenga ya nyuki kuweka asali na wakati wa kurina asali nyuki wahadhuriki.
“Tumeanza majaribio na tayari makundi ya nyuki yameanza kuingia katika mizinga hii na tukiona ufanisi mkubwa tutaanza kuwapa wafugaji”anasema
Akizungumzia miradi ya Nyuki waliyonayo anasema mwaka 2026, FCF imewezesha vikundi vya ufugaji nyuki zaidi ya 16.
Mabula anasema vikundi hivyo vina Watu 699 kati yao Wanaume 119 na Wanawake 244 .
“Msimu wa 2025-2026: Tani 4.27 za asali zilivunwa”anasema
Akizungumzia mradi wa Stadi za Maisha na Elimu ya Mazingira Mashuleni Mabula anasema Wanafunzi 4,822 kwenye klabu za shule wamefundishwa elimu ya mazingira kati yao Wavulana 2,394 na Wasichana 2,428.
“Wanafunzi 2,445 walipata mafunzo ya stadi za maisha kati ya Wavulana 775 na Wasichana 1,670″anasema
Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo ,Kaimu Mkurugenzi halmashauri ya Meatu Protas Dibogo amepongeza Friedkin kwa kuja na technolojia ya Mizinga ya Plastiki.
Friedkin Conservation Fund (FCF) ni wadhamini waliosajiliwa wanaotekeleza kazi za kijamii kwa niaba ya kampuno ya Utalii na Uhifadhi ya Mwiba Holdings Ltd katika jamii zinazozunguka Pori la Akiba la Maswa.







