Rais wa Jumhuri ya Burundi Mheshimiwa Évariste Ndayishimiye amewasili katika Uwanja wa Ndega wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Mkoani Kilimanjaro, kushiriki katika Mkutano wa 25 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaofanyika leo tarehe 7 Machi 2026 katika Makao Makuu ya Jumuiya jijini Arusha.
Akiwasili Mkoani humo amepokelewa na Mhe. Mahmoud Thabit Kombo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiambatana Viongozi Waandamizi mbalimbali wa Serikali.













