Kikosi cha Polisi Tanzania kimeendelea na Maandalizi kabambe kuwakabili Songea United katika mchezo wa Ligi ya Championship utakaochezwa Jumamosi Mei 2, 2026 katika uwanja wa Ushirika – Moshi mkoani Kilimanjaro.
Afisa habari wa kikosi hicho, Inspekta Frank Lukwaro amesema maandalizi yao yanaendelea vyema na wanatambua ugumu wa mchezo kutokana na aina ya timu wanayokutana nayo.
Lukwaro amesema wanamheshimu kila mpinzani bila kujali nafasi aliyopo kwa kuwa timu zote zipo katika ligi moja na hakuna inayopenda kupoteza mchezo kirahisi hivyo wataingia kwa kuwaheshimu Songea ambapo wapo nafasi ya saba katika msimamo huku Polisi ikiwa nafasi ya nne.
Aidha, Lukwaro amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi ili kuendelea kutoa sapoti, jambo ambalo litaongeza chachu ya kupata ushindi.
Kwa upande wake Mwalimu wa Kikosi hicho Mbwana Makata amesema amekiandaa vizuri kikosi chake ili kupata matokeo chanya katika mchezo wa kesho.


