Jeshi la Polisi Tanzania lingependa kujulisha kuwa, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura, amemhamisha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Twaha Juma Lulengelule ambaye alikuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) Mkoa wa Tabora kuwa Kamanda wa Polisi (RPC) Mkoa wa Tabora.

Uhamisho huo umefanyika ili kujaza nafasi iliyokuwa wazi baada ya aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa huo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Richard George Abwao, kufariki dunia Juni 20, 2026.