Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia
Dar es Salaam

CRDB Benki imeendesha droo ya kampeni ya “SimBanking Kimpango Wako” na kuwapata washindi wa zawadi mbalimbali, ikiwemo watano waliojishindia safari ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mshindi mmoja wa friji aina ya Double Door pamoja na washindi 10 wa Smart TV za inchi 65.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Julai 6, 2026, wakati wa kutangaza washindi hao, Meneja wa SimBanking wa CRDB, Amina Mawuna, alisema droo hiyo huendeshwa kila baada ya miezi mitatu kwa lengo la kuwazawadia wateja wanaotumia huduma ya SimBanking kufanya malipo na miamala mbalimbali wanaponunua bidhaa na huduma.

Alisema katika droo hiyo washindi watano wamejishindia safari ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, mshindi mmoja amejishindia friji aina ya Double Door, huku washindi 10 wakijishindia Smart TV za inchi 65.

Kwa upande wake, Influencer wa CRDB, Eliud Samweli, amesema mchakato wa kuwapata washindi umefanyika kwa uwazi na bila upendeleo, kwani droo hiyo huchezeshwa mubashara kupitia ukurasa wa Instagram wa CRDB, jambo linalowapa wateja nafasi ya kushuhudia zoezi zima.