Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), kimesisitiza umuhimu wa kuwajengea uwezo vijana 40 wanaofanya kazi katika sekta ya habari kote nchini Tanzania, ili waweze kuandika habari za mabadiliko ya tabianchi wakizingatia Maarifa (Dhana, Sifa, Aina za maudhui, Dhana ya Uwajibikaji, Mbinu kuu), Matendo (Maswali Makuu, Kanuni Kuu na Zana za Msingi zakuzilisha Bidhaa) na Matokeo (Jinsi ya kufuatilia na kurekodi matokeo).
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa JET, John Chikomo, alipokuwa akitoa salamu za ufunguzi kwenye Uzinduzi Rasmi wa Kundi la Pili la Mpango wa Utetezi wa Media4Climate; mpango ulioundwa ili kuwajengea uwezo vijana 40 wanaofanya kazi katika sekta ya habari kote nchini Tanzania iliyofanyika leo tarehe 28 Julai, 2026 katika Ukumbi wa UN House jijini Dar es Salaam.

Warsha hiyo iliandaliwa kupitia Mradi wa MEDIA4CLIMATE Advocacy Initiative unaotekelezwa na Youth Survival Organization (YSO Tanzania), kwa ufadhili wa Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa (UNEP).
Lengo la warsha hiyo lilikuwa Uzinduzi Rasmi wa Kundi la Pili la Mpango wa Utetezi wa Media4Climate; mpango ulioundwa ili kuwajengea uwezo vijana 40 wanaofanya kazi katika sekta ya habari kote nchini Tanzania, kwa kuwapa ujuzi wa kuhabarisha jamii wanazozihudumia kuhusu sayansi ya mabadiliko ya tabianchi, sera za kitaifa, na majadiliano ya kimataifa kuhusu tabianchi.
Lakini pia kuwajengea uwezo vijana hao 40 waweze kushiriki kikamilifu katika kuandika habari za COP31 ambao ni Mkutano wa 31 wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi, unaotarajiwa kufanyika katika Kituo cha Antalya EXPO mjini Antalya, Uturuki, kuanzia tarehe 9 Novemba hadi 20 Novemba 2026.
Kundi hili linajenga juu ya msingi imara na matokeo dhahiri yaliyopatikana kupitia kundi letu la kwanza, lililopata mafunzo mwaka 2024.

Katika wasilisho lake, Chikomo alieleza mchango wa JET katika uhifadhi wa mazingira kupitiauandishi wa habari za mazingira, kampeni za uhamasishaji wa umma pamoja na matumizi ya vyombo vya habari katika kuongeza uelewa wa jamii kuhusu masuala ya mazingira.
Aidha, alibainisha kuwa JET ina jukumu la kuwakilisha waandishi wa habari za mazingira na sauti za asasi za kiraia katika mkutano wa COP31 pamoja na michakato mingine ya kimataifa inayohusu mazingira.
Alisema waandishi wa habari wana nafasi muhimu katika kushughulikia changamoto za mazingira kwa kuongeza uelewa wa wananchi, kusaidia utekelezaji wa miradi ya uhifadhi wa mazingira, kujenga uwezo wa jamii na kutetea sera zinazolinda mifumo ikolojia iliyo hatarini huku zikihamasisha usimamizi endelevu na wenye usawa wa rasilimali asilia.
Tukio hilo liliwakutanisha wawakilishi kutoka taasisi asasi za kiraia, washirika wa maendeleo na wadau wa mazingira, ambao walisisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano katika mapambano dhidi ya Mabadiliko ya Tabianchi nchini.
Warsha hiyo ilifunguliwa rasmi na Clara Makenya mwakilishi wa UNEP nchini Tanzania ambaye alitoa wito wa kuimarishwa kwa ushirikiano kati ya serikali, waandishi wa habari asasi za kiraia na wadau wengine katika jamii wanazozihudumia kuhusu sayansi ya mabadiliko ya tabianchi, sera za kitaifa, na majadiliano ya kimataifa kuhusu tabianchi.





