Na Mwandishi Wetu,JamhuriMedia, Dar es Salaam

Dar es Salaam

BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza kuwa msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, maarufu kama NBC Premier League, kwa mwaka 2026/2027 unatarajiwa kuanza rasmi Oktoba 29, 2026 na kuhitimishwa Mei 27, 2027.

Taarifa hiyo imetolewa leo Agosti 28, 2026, jijini Dar es Salaam na Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Cornel Barnabas, wakati akizungumza kuhusu maandalizi ya msimu mpya wa ligi hiyo.

Barnabas amesema ratiba ya msimu huo imeandaliwa kwa kutumia mfumo wa kidijitali, hatua inayolenga kuhakikisha upangaji wa michezo unakuwa wenye ufanisi na kuzingatia mahitaji ya mashindano.

“Ratiba imeandaliwa kidijitali, hivyo nazitakia maandalizi mema timu zote zitakazoshiriki katika mtanange huo,” amesema Barnabas.

Kutangazwa kwa tarehe hiyo kunatoa mwanga kwa klabu zinazoshiriki NBC Premier League kuendelea na maandalizi yao kuelekea msimu mpya, huku mashabiki wa soka nchini wakisubiri kwa hamu kuanza kwa ushindani mwingine wa kuwania ubingwa.

Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali za ratiba za msimu wa 2026/2027, mashindano ya NBC Premier League yanaendelea kuwa miongoni mwa yanayofuatiliwa kwa karibu katika soka la Tanzania.

Afisa Habari wa TPLB,Yahaya Abusheh Amesema Timu zitakazoshiriki ni 16 ambapo kutakuwa na makundi mawili kundi A kutakuwa na Timu 8 huku B 8