Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Pwani
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPPC), David Kafulila, amefafanua kuwa uamuzi wa kuanzia Mkoa wa Pwani katika uzinduzi wa Kongamano la Fursa za Uwekezaji kupitia PPP haukufanyika kwa bahati mbaya, bali umetokana na tathmini ya kina ya uwezo wa kipekee wa mkoa huo.
Kafulila ametoa kauli hiyo Ijumaa, Septemba 25, 2026, mjini Kibaha, mkoani Pwani, wakati wa uzinduzi wa Kongamano la Fursa a Uwekeaji Kupitia PPP, lililofanyika mkoani humo.
Alisema Pwani haipaswi kutazamwa kama mkoa wa kawaida, bali kama nchi yenye uchumi wake binafsi, na kubainisha kuwa mkoa huo una ukubwa wa kilomita za mraba 33,000.
Kafulila alisema kama Pwani ingekuwa nchi huru, ingeshika nafasi ya 139 kati ya nchi 193 wanachama wa Umoja wa Mataifa kwa
Hata hivyo, Kafulila alitumia methali ya Kiswahili isemayo, “Ukikaa karibu na waridi lazima unukie”, kueleza kuwa Pwani ndiyo mkoa unaonufaika zaidi na uwepo wa Dar es Salaam kuliko mkoa mwingine wowote
“Vietnam inakua kwa kasi kwa sababu iko karibu na China, huku Korea Kusini, Japan na Singapore zikikua kwa sababu ziko katika maeneo yenye fursa kubwa za biashara za kimataifa,” alitoa mifano hiyo kuunga mkono nadharia aliyoisema.
Kwa mantiki hiyo hiyo, alisema Pwani inapaswa kuitumia Dar es Salaam kama Singapore inavyotumia bahari kama lango la biashara.
“Pwani ina bahati ya kuwa na rasilimali tatu ambazo hakuna mkoa mwingine nchini unazo kwa pamoja ikiwemo Kisiwa cha Mafia, ambacho ni kisiwa cha tatu kwa ukubwa nchini Tanzania, chenye ukubwa wa kilomita za mraba 394,” alisema.
“Pili ni Bwawa la Julius Nyerere, ambalo peke yake lina ukubwa wa kilomita za mraba 530, sawa na asilimia 90 ya eneo lote la Jiji la Dar es Salaam and tatu ni Mto Rufiji,ambao ni mkubwa nchini,” alisema.
Kafulila alisema mto huo humwaga maji yake Bahari ya Hindi kwa takriban lita trilioni nane za maji kila mwaka, na kubainisha kuwa maji hayo yanapotea baharini bila matumizi yoyote ya kiuchumi.
“Maji hayo hayapaswi kuendelea kupotea, bali yanapaswa kugeuzwa kuwa rasilimali ya kiuchumi kupitia miradi ya PPP,” alisema


