Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Arusha Mjini, Paul Makonda, ametoa wito kwa wananchi wa Arusha kutumia fursa ya huduma za uchunguzi na upimaji wa saratani zinazotolewa kwa ushirikiano kati ya Ocean Road Cancer Institute (ORCI), Ofisi ya Mbunge wa Arusha Mjini na Hospitali ya Kaloleni.
Makonda amesema katika kambi iliyopita, wananchi walipatiwa huduma za uchunguzi na matibabu, huku baadhi yao wakibainika kuwa na viashiria vilivyohitaji ufuatiliaji na hatua zaidi za kitabibu.
Amesema ushirikiano huo unaendelea tena Arusha, akiwataka wananchi kutoka kata mbalimbali kujitokeza na kutumia fursa hiyo kupima afya zao mapema.
“Hatuna sababu ya kusubiri mpaka ugonjwa uwe mkubwa. Ukipima mapema na tatizo likabainika, hatua za matibabu zinaweza kuanza mapema.”

”




