
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi,akisalimiana na kutowa mkono wa pole kwa Familia ya Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhajj Dkt.Salmini Amour Juma, baada ya kumalizika kwa kisomo cha hitma na dua ya kumuombea Marehemu Hamisa Salmini Amour, iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akijumuika na Wananchi katika kisomo cha hitma kumuombea Marehemu Hamisa Salmini Amour, Mtoto wa Rais Mstaafu wa Zanzibar Alhajj Dkt.Salmini Amour Juma iliyofanyika katika Masjid Jamiu Zinjibar Mazizini Zanzibar, na (kushoto kwa Rais) Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh.Hassan Othman Ngwali na (kulia kwa Rais) Amini Salmini Amour.(Picha na Ikulu)
