Mashambulizi kadhaa ya anga ya jeshi la Israel kwenye Ukanda wa Gaza yameuwa takribani watu 30 na kuwajeruhi wengine kadhaa.
Kwenye mashambulizi ya hivi karibuni zaidi, watu kumi wameuawa usiku wa kuamkia leo na zaidi ya 50 wamejeruhiwa, kwa mujibu wa mashahidi na wafanyakazi wa Hospitali ya Nasser.
Hayo ni baada ya jeshi la Israel kulishambulia kwa makombora hema la wakimbizi wa ndani kwenye eneo la Al-Mawasi katika kitongoji cha Khan Younis.
Watu sita miongoni mwa waliouawa walikuwa wa familia moja. Mashambulizi ya awali kaskazini mwaGazayaliuwa watu 17, ambapo mkurugenzi wa Hospitali ya Indonesia na familia yake nzima ni miongoni mwa waliouawa.
Jeshi la Israel halijasema chochote kuhusu mauaji haya.
