Nchi za Afrika kwa ujumla wake zimefanikiwa kupata ushindi kwa zaidi ya mechi 3 katika hatua ya makundi ya Kombe la Dunia ambapo katika Michuano ya Kombe la Dunia inayoendelea nchini Qatar nchi za Afrika zimepata ushindi katika mechi 4.  

Nchi za Afrika ambazo zimepata ushindi mpaka sasa katika michuano hiyo ni Tunisia ambao waliwafunga Ufaransa 1-0, Senegal walipata ushindi 2-1 dhidi ya Equador, Morocco waliichapa Ubelgiji 2-0 na Ghana waliiadhibu Korea Kusini magoli 3-2. 

Mpaka sasa nchi pekee ya Afrika ambayo haijaandikisha ushindi katika michuano hiyo ni Cameroon pekee. Rekodi nyingine iliyovunjwa ni pamoja na kuweza kujikusanyia point 18 katika michuano ya Kombe la Dunia ya awamu moja pekee ambapo rekodi kubwa ilikuwa ni kukusanya point 15 katika michuano ya awamu moja. 

Jambo la kusisimua ni kuwa nchi za Afrika bado zina mechi nyingine za kucheza huku kukiwa na matumaini ya kuvunja rekodi zaidi na zaidi ikiwa morali na kujituma kwa timu za Afrika kutaongezeka zaidi. 

By Jamhuri