Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Tabora

Uongozi wa Shirika la Akili platfom Tanzania kwa kushirikiana na vijana kutoka vyuoni wamefika katika kituo cha wazee Ipuli kwa jina lilizoeleka Kijiji cha Amani mkoani Tabora kwa zoezi la kutenda

Zoezi hilo limefanyika Januari 6, 2024 kwa kupanda miti jumla 145 ya matunda na migomba kweny bustani ya kituo hicho.

Mkurugenzi Mtendaji Akili platfom Tanzania Ceo.Mc.Mwalimu Roghat Robert amesema lengo la kuweka siku hii adhimu kufanya hiyo shughuli ni,kufungua mwaka 2024 kwa kupata baraka za wazee, kupanda miti ambayo itatoa faida kwa wazee hasa kuwapatia matunda, kivuli, hewa safi na kuzuia mmonyonyoko wa ardhi.

Pia kutoa mwangaza kuwa matendo ya huruma ni sehemu ya ibada na kazi za mikono kwani kupitia kufanya kazi hufungua mwanya zaidi, kuwafariji wazee na kuwatakia maisha marefu kwa mwaka huu wa 2024 , kuonyesha mchango wa vijana katika kusaidia wenye uhitaji maalum akitolea mfano wa vijana kutoka chuo kikuu cha AMUCTA, TPSC na chuo cha ARIDHI Tabora ambao ni chachu kuu ya kuonyesha faraja, matumaini, amani na kwa wenye uhitaji.

Pendo Chiryamkubi akisema,
ujumbe kwa vijana kwa mwaka 2024 mlioufungua kwa baraka hizi za kutembelea kituo chetu.

“Vijana mnatakiwa kuendelea kutambua dhamana na wajibu wenu katika kusaidia wazee na makundi mengine maalum katika jamii” amesema.

Hivi leo vijana kutoka Shirika letu pendwa sana linaloongozwa na vijana wadogo ila mambo makubwa la AKILI PLATFORM TANZANIA mmeonyesha mfano bora wa kuigwa kwa kuweka alama katika kituo cha wazee na wasiojiweza kwa kupanda miti ya matunda itakayosaidia kupata matunda, kivuli na hewa ndani ya kituo chetu.

Amesema kwa kufanya hivyo ni alama isiofutika na haijawahi tokea tangu kituo kuanzinshwa hivyo atafikisha taarifa hiyo wizarani watambue walivyofungua mwaka 2024 kwa ubunifu mkubwa sana.

“umuombee kiongozi wetu Bw. Roghat Robert ambaye amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kjwa kituo hicho kinatimizs malengo yake kwa ushirikiano na wanachama na vikngozi mbalimbali wa ndani na nje ya kituo.

Naye mwenyekiti wa Mtaa wa Uredi, John Mwanda amefurahia ustawi wa vijana katika matendo ya huruma na kusema hii ni tunu na hazina daima na ameomba kupandiwa miti mingine kwenye shule zake na kuhakikisha miti iliyopandwa anaisimamia vyema na inazaa matunda chanya.

Naye mzee Mzee Edward Sonda amesema baraka ziwashukie kila kijana na watu wazima waliweza kujitoa katika kufanikisha shughuli ya kuwawekea bustani kama ya Adam aliyokuwa akisimamia hivyo kwa niaba ya wazee aliwashukuru sana kwa jinsi walivyofanikisha shughuli hiyo.

Upendo msimamizi wa kituo cha wazee amesema hakika imekuwa neema kwani Serikali imeshaandaa mazingira ya kuwajengea nyumba wazee na zaidi miti ya matunda itasaidia katika eneo la lishe ikisha stawi vizuri.

Zaidi italeta mazingira mazuri kwani hakuna aliyeweza kuleta bustani zaidi ya wadau wa Akili platfom Tanzania kwa kweli Mungu awape maisha marefu.

Hata hivyo aliwaomba sana kuendelea kuitunza kwa pamoja kwani haitakufa pia kuendelea kupanda miti zaidi kwani bado kuna uhitaji ni mkubwa sana hasa hii ya matunda.