Na isri Mohamed

DAKIKA 90 za mtanange wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Simba vs AL Ahly ya Misri zimemalizika kwa mnyama kukubali kichapo cha bao moja kwa Nunge lililofungwa kipindi cha kwanza.

Kocha mkuu wa Simba, Abdelhak Benchika amezungumza kwa uchungu mbele ya waandishi wa Habari akisikitika kwanini wachezaji wake wameshindwa kupata goli licha ya kutengeneza nafasi nyingi kuliko AL Ahly.

“Tumefika sana langoni kwao, lakini sijui kwanini wachezaji wangu wameshindwa kufunga, inaumiza sana, tutajitahidi kufunga kwenye mechi ya marudiano kwao”

“Naiandaa timu yangu kupata ushindi Misri, haijalishi tutacheza katika uwanja gani, Mpira ndivyo ulivyo, Nimeshacheza sana na AL Ahly, Nitaiandaa tena timu yangu na tutapata ushindi”

Mechi ya Marudiano kati itachezwa Aprili 05, katika dimba la Cairo International nchini Misri.