Al-Shabab kuondolewa Somalia

Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud amesema taifa hilo lina muda wa mwaka mmoja kuliondoa kundi la wanamgambo wa Al-Shabaab

Agizo hilo limekuja huku muda wa mwisho wa wanajeshi waliosalia wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika kuondoka ukikaribia mwezi Disemba.

Mohamud, akihudumu muhula wake wa pili kama rais, alisema mwezi Agosti alitaka kuuondoa mapema kufikia mwaka ujao.

“Mwisho ni Disemba 2024 wakati vikosi vyote vya ATMIS (vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Afrika) vinapaswa kuondoka nchini,” Mohamud aliiambia.