Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Moshi

Lucas Paul Tarimo, aliyekuwa akituhumiwa kumchoma visu mkewe mara 25 marehemu Beatrice Minja (45), mkazi wa kijiji cha Mbomai juu, Kata ya Tarakea mkoani Kilimanjaro, naye amefariki.

Marehemu alikamatwa akiwa amejificha katika Kijiji cha Jema Kata ya Oldonyo Sambu Wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha akijiandaa kukimbilia nchi jirani.

Kwa mujibu wa msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime, alisema kuwa marehemu baada ya kuona mkono wa Serikali unamfikia alikunywa sumu inayotumika kuua wadudu ambapo baada ya kukamatwa alikimbizwa hospitali.

Marehemu huyo anadaiwa kumchoma kisu mara 25 marehemu mkewe ambapo alikaa ICU kwa siku 46 katika Hospitali ya KCMC.

Marehemu Beatrice Minja alishambuliwa siku ya Novemba 12 mwaka jana katika kijiji hicho, majira ya jioni alipokua akitokea katika majukumu yake na mtu ambaye mpka sasa hajakamatwa na jeshi la polisi.

Kwa mujibu wa mtoto wa marehemu, amesema mama yake alikua akifuatiliwa na kupewa vitisho na mtuhumiwa huyo na aliripoti kituo cha Polisi lakini aliachiwa kwa dhamana na aliendelea na vitisho na baadae mama yake kujeruhiwa.

Fuatilia zaidi taarifa kuhusiana na habari hiyo baadaye.

Marehemu Beatrice Minja
Marehemu Lucas Paul Tarimo