Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Arusha

Bodi ya Nyama nchini (TMB), imeendelea kutoa mafunzo kwa wadau wa tasnia ya nyama kama inavyoekeleza sheria ya nyama namba 10 ya Mwaka 2006 ambayo ilizinduliwa Novemba 14, 2008 ikiwa na lengo la kuweka mazingira bora ya uzalishaji na usindikaji wa wanyama kwa kuzingatia viwango vya ubora ili kukidhi mahitaji ya soko la ndani na nje.

Akiongea mara baada ya mafunzo hayo leo Januari 0l3,2024, Afsa Abdallah Milandu ambaye ni Msimamizi wa Idara Inayohusiana na Usajili na Udhibiti Ubora Bodi ya Nyama nchini amesema kuwa wamekutana na wadau wa Tasnia ya nyama lengo likiwa ni kuwaelekeza kuhusiana na Muongozo wa uzalishaji na uandaji wa nyama katika maduka yao.

Afsa ameongeza kuwa lengo la bodi hiyo ni kutoa elimu kwa wote ili wauzaji na walaji wa nyama wanufaike kwa kupata nyama bora na salama huku akiwataka wadau hao kutambua kuwa tayari mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan alishafungua milango ya masoko ambayo itaboresha zaidi tasnia hiyo ya nyama.

Sambamba na hilo ametoa rai kwa wadau hao na wengine ambao hawata pata mafunzo hayo ambayo yatatolewa nchi nzima kwa kipindi husika huku akibanisha kuwa ambao watapata mafunzo hayo hawatoruhusiwa kufanya biashara hiyo.

Godfrey Kakuru ambaye ni mwenzeshaji kutoka Bodi ya Nyama nlnchini (TMB) amewataka wadau wa Tasnia ya nyama kutambua nyama bora ni ile ambayo inatoka katika mfugo salama usio na chembechembe ya dawa na ile ambayo imefuata taratibu ya utambuzi kutoka kwa wataalam wa mifugo.

Nae Afisa mfawidhi wa bodi hiyo Kanda ya Kaskazini Bw. Patrick Kaaya amesema kuwa wamezindua mafunzo hayo kanda ya kaskazini ambapo amebainisha kuwa mafunzo hayo yamelenga kuweka mazingira salama ya wauzaji na watumiaji wa nyama wa mikoa ya Arusha,Kilimanjaro,Manyara na Tanga.

Nao baadhi ya wadau wa tasnia ya nyama mkoani Arusha wamesema elimu hiyo imekuja wakati sahihi ambapo wamebanisha kuwa kuna ongezeko la walaji wa nyama huku mdau mwingine wa Tasnia ya nyama akiomba bodi hiyo kusimamia kikamilifu milipuko ya maduka ya nyama yasio na

By Jamhuri