Wachina wamkunja Meya Dar
Kampuni ya Ujenzi ya Tanpile Ltd ya China inalalamikiwa na wananchi waishio katikati ya Jiji la Dar es Salaam kwa uchafuzi wa mazingira na kelele usiku kucha, zinazosababisha washindwe kupumzika, JAMHURI inaripoti. Kampuni hiyo licha ya kupewa amri ya Mahakama (stop order) kusitisha shughuli zake za uchanganyaji wa zege katika kiwanda chake kilichofunguliwa katika makutano…