JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Author: Jamhuri

Ndugu Rais maisha haya mpaka lini?

Ndugu Rais, alianza waziri akasema ameshangaa kuona baadhi ya Watanzania wakishangilia kuzuiwa kwa ndege ya ATCL nchini Afrika Kusini. Hajawahi kuona sherehe msibani. Ashibae hamjui mwenye njaa – lazima ashangae. Inapotokea hata Katibu Mkuu wa CCM, Bashiru Ally, naye ameshangazwa…

Tusipotoshe kauli tukaiharibu nchi (2)

Sehemu iliyopita, mwandishi wa makala hii alinukuu maneno kutoka kwenye kitabu kilichoandikwa na Mohammed Said, yaliyohusu hofu aliyokuwa nayo mmoja wa wana TANU, Sheikh Takadir, juu ya TANU kumezwa na Ukristo. Endelea… Hapo waweza kuona mbegu ya uhasama wa kidini…

Nini maana ya utumishi wa umma?

Tukio la hivi karibuni limenisukuma kutafakari ni nini maana nzuri ya utumishi wa umma, na ni nini unapaswa kuwa uhusiano wa mtumishi wa umma na jamii yake. Kwenye hoja yangu najumuisha watumishi wa kuchaguliwa na wa kuteuliwa kwa sababu, aghalabu,…

Kwanini Bageni anyongwe peke yake kati ya watu 13? (2)

Toleo lililopita tuliishia aya inayosema: “Kwa msingi huu, Mahakama Kuu haikumuona Bageni akifyatua risasi, kwa sababu si yeye aliyefyatua risasi, hivyo upande huo akaondolewa, lakini pia haikumuona akiamrisha risasi kufyatuliwa, kwa sababu aliyefyatua hakuwapo mahakamani kumtaja kuwa ndiye akiyemwamrisha kufyataua,…

Ukipoteza muda, muda utakupoteza zaidi (2)

Wiki iliyopita makala hii iliishia pale ambapo ilikuwa inasomeka: ‘hauwezi ukashinda kama hauchezi, mwanadamu anaishi mara moja tu hapa duniani. Tunaloweza kulifanya sasa, tulifanye kwa sababu hatuishi mara ya pili hapa duniani. Kubahatika kuishi duniani ni fursa.’ Endelea… Ni fursa ya…

MAISHA NI MTIHANI (44)

Maneno ‘asante sana’ yanaroga mtoaji atoe zaidi Shukrani ni mtihani. Kwa mtazamo wangu, shukrani ni utajiri, kutoshukuru ni umaskini. Shukrani ni furaha, kutoshukuru ni huzuni. Shukrani ni fadhila, kutoshukuru ni kilema. Shukrani ni chanya, kutoshukuru ni hasi. Shukrani ni kicheko,…