Na Abel Paul,JamhuriMedia,Arusha

Uongozi wa Wilaya ya Arusha umewaka waenda Pikipiki za mataili matatu maarufu bajaji kufuata utaratibu na kuweka mipango mathubuti wa uendeshaji wa shughuli zao katika jiji la Arusha ambapo wametakiwa kujisajili na kuweka uongozi imara ili kuondoa dhana ya kuwa kundi hilo ni la watu wasiojitambua.

Akifungua kikao hicho leo Oktoba 15,2022 kilicho hudhuliwa na bajaji zaidi ya 700 Mkuu wa Wilaya ya Arusha Bw.Said Mtanda ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama Wilaya Arusha amebanisha kuwa kuwa serikali ina mipango ya dhabiti na waendesha bajaji ambapo amewataka kuchagua viongozi imara na kufuata taratibu zilizopo ili kuto kizana na serkali.

Mtanda amebainisha kuwa kuanzia leo Serikali katika Halamashauri ya Jiji la Arusha imesitisha hutoaji wa leseni mpya za LATRA ndani ya jiji la Arusha ambapo amebainisha kuwa kwa sasa wameanza kusajili maeneo rasmi ambayo madereva hao watafanya shughuli zao.

Kwa upande wake Mkuu wa kikosi cha usalama Barabarani Mkoa wa Arusha Mrakibu wa Polisi SP-Solomon Mwangamilo amesema Jeshi la Polisi kupitia kikosi cha usalama barabarani kimepokea maelekezo ya serikali katika kusimamia mikakati mipya ya kuboresha na kusimamia waendesha bajaji katika jiji la Arusha.

Naye kaimu Mkurungenzi wa Jiji la Arusha Bw.Hargeney Chitukuro amesema kuwa wao kama halmashauri ya jiji la Arusha hawana ugomvi na waendesha bajiji ambapo amewataka kufuata sheria na taratibu zilizowekwa.

Aidha kwa upande wake afisa Latra Mkoa wa Arusha Bw.Amani Mwakalebela amesma kuwa kuwa wataendelea kutoa elimu ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua kwa madereva wote watakao kiuka sheria na taratibu za usalama barabarani katika Mkoa wa Arusha.

Pia kwa upande wake mwanasheria wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Bw.Idd Ndabona amesema sheria za halmashauri ya jiji la Arusha ziko wazi kwa waendesha bajaiji ambapo amebainisha kuwa wao wanashirikina na LATRA katika kutoa dira na kusimamia ikiwa ni Pamoja na kusajili vyombo hivyo.

Nao baadhi ya waendesha bajaji katika jiji la Arusha wameshukuru serikali kwa kuwapa dira sahihi katika kazi zao za kila siku nakuomba serikali kusimamia jambo hilo

By Jamhuri