Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Hamis Kigwangalla amepata ajali katika eneo la Magugu mkoani Manyara. Waziri Kigwangalla amejeruhiwa maeneo mbalimbali ya mwili wake, huku mwanahabari Hamza Temba akifariki dunia.

Waziri Kigwangalla alikuwa katika ziara ya kikazi ambapo alikuwa akikagua utendaji kazi wa watendaji na mamlaka zilizopo chini yake pamoja na mapori mbalimbali nchini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Augustino Senga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Taarifa za awali kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa, Waziri Kigwangalla alikuwa akisubiria helikopta ili awahiswe hospitali.

Hapa chini ni picha za ajali hiyo:

Please follow and like us:
Pin Share