Mmiliki wa kampuni ya Lugumi, Said Lugumi leo asubuhi Jumanne Julai 31, 2018 amejisalimisha katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani jijini Dar es Salaam kuitikia wito wa waziri wa wizara hiyo, Kangi Lugola.
Julai 21, 2018 Lugola alimpa siku 10 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro kumfikisha Lugumi ofisini kwake ifikapo leo, saa 2 asubuhi.
Siku hiyo, Lugola alisema kampuni ya Lugumi ilipewa zabuni ya kufunga vifaa vya utambuzi wa alama za vidole kwenye baadhi ya vituo vya polisi baina yake na jeshi la polisi, lakini hakukamilisha kazi hiyo.
Kampuni ya Lugumi iliingia mkataba wa Sh37bilioni za Jeshi la Polisi kufunga mashine za kieletroniki za kuchukua alama za vidole katika vituo vya jeshi hilo, lakini ilibainika kutotimiza masharti baada ya kufunga mashine 14 kati ya 106, licha ya kulipwa asilimia 90 ya fedha, kwa mujibu wa mkataba.

#mwananchi

Please follow and like us:
Pin Share