Leo tarehe 20 Mei 2024, Phaustine Kasike, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amekutana na Alcinda António de Abreu, Mjumbe wa Kamisheni ya Siasa ya Chama cha FRELIMO.

Kupitia mkutano huo uliofanyika kwenye Ofisi za Makao Makuu ya FRELIMO zilizopo jijini Maputo, viongozi hao wawili walizungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na Msumbiji na kukubaliana juu ya umuhimu kwa uhusiano huo kuendelezwa kwa maslahi ya nchi zetu mbili.

Kwa upande mwingine,Balozi Phaustine alikipongeza Chama cha FRELIMO kwa kumaliza mchakato wa kumpata mgombea wake wa nafasi ya Urais kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 09 Oktoba, 2024 ambapo Daniel Francisco Chapo aliteuliwa kupeperisha bendera ya Chama hicho.