Waziri wa Kilimo Mheshimiwa Hussein Bashe (Mb) amewataka wakurugenzi wa Halmashauri zote nchi kuhakikisha maafisa Ugani wanapatikana katika vituo vyao vya Kazi kama ilivyo kwa walimu. Bashe ameyasema hayo leo hii akiwa mkoani Tanga ambapo ameanza ziara yake ya kikazi ya siku tatu.

Bashe amesema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uwekezaji mkubwa katika utekelezaji wa Ajenda 10/30 kilimo biashara kwa kuwanunulia maafisa ugani wote nchini pikipiki, vishikwambi , Vipima afya ya udongo na lamination machine na kuanza utekelezaji wa kuwajengea nyumba katika vituo vyao vya kazi walipo wakulima.

Aidha amesisitiza kuwa maafisa ugani wote wawe na mfumo wa kutoa taarifa ya utekelezaji wao wa majukumu ikiwemo kutoa taarifa za wakulima walio watembelea na changamoto walizozitatua kwani wizara ya kilimo haitomvumilia afisa ugani yeyote asie endana na kasi hii ya utekelezaji wa malengo mapana ya serikali.