Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamtafuta dereva wa gari namba T904 DKY Kampuni ya Abood kwa kosa la kugonga gari aina ya Noah lenye namba za usajili T828 DNB na  kusababisha ajali  iliyouwa watu wawili na wengine wawili kujeruhiwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama, amesema kuwa ajali hiyo imetokea Septemba 11, 2023 majira ya saa tatu, asubuhi Barabra Kuu ya Dar es Salaam – Morogoro maeneo ya Kingolwira Manispaa ya Morogoro ambapo chanzo cha ajali ni matumizi mabaya ya barabara, dereva wa basi alicha upande wake na kutumia upande mwingine na kuigonga Noah.

Scolastica Solomon, Kaim Afisa Uhusiano Hospatali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro, akizungumza kwa niaba ya Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo amesema wamepokea majeruhi wawili waliofahamika kwa majina ya Ally Sarehe na Shabani Salumu Mdango na miili miwili ya marehemu ambapo ammoja amefamika kwa majina ya Safiri Kibwana huku mwingine akiwa bado hajatambulika.