Rais Joe Biden anaendelea kukabiliwa na wito wa kujitoa kwenye kinyang’anyiro cha urais na kumpisha mgombea mwengine wa chama chake kupambana na Donald Trump kwenye uchaguzi wa Novemba mwaka huu.

Magavana na wabunge kadhaa wa chama chake wanangoja mahojiano ya Biden na kituo cha utangazaji cha ABC baadaye leo, kuamua ikiwa waendelee kumuunga mkono ama la.

Shinikizo hili la sasa linatokana na kushindwa vibaya kwa Biden kwenye mdahalo wake na Trump wiki iliyopita.

Makamu wake, Kamala Harris, anaangaliwa na wengi kwamba ndiye atakayewania urais, endapo Biden atalazimika kujitowa.

Hata hivyo, Ikulu ya White House imesema kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 81 hana mpango wa kuchukuwa hatua hiyo.