Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir amemfukuza kazi Waziri wa Fedha Awow Daniel Chuong ambae amehudumu katika nafasi hiyo kwa kipindi cha miezi minne, huku sababu za uwamuzi huo hazikuwekwa hadharani.

Katika miaka ya hivi karibuni, Uchumi wa Sudan Kusini umekuwa ukisuasua, huku kukishuhudiwa kwa changamoto chungumzima ikiwemo ghasia za kikabila, mapato ya mauzo ya mafuta ghafi yakipungua tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vya mwaka 2013 hadi 2018, na kutatizika kwa mauzo ya nje kutokana na vita vinavyoendelea katika nchi jirani ya Sudan.

Kiir alichaguliwa kuwa rais wa kwanza wa Sudan Kusini mwaka 2011, wakati nchi hiyo ilipojipatia uhuru wake kutoka Sudan. Nchi hiyo inatarajia kufanya uchaguzi wake mkuu mwezi Desemba.